Bandari College
+255-22-2857114   pbc@ports.go.tz

Wahadhiri kutoka Chuo cha Bahari cha Busitema (Busitema University Maritime Institute) cha nchini Uganda kimeanza ziara ya siku nne (4) katika Chuo cha Bandari yenye lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za Kitaaluma.

Aidha, ziara hii ina lengo la kuanzisha njia za ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa kuandaa na kuhuisha mitaala. Ugeni huu umepokelewa na Menejimenti ya Chuo cha Bandari, ikiongozwa na Mkuu wa Chuo Dkt. Lufunyo Hussein.

Katika mapokezi hayo, Dkt. Lufunyo alifafanua na kusisitiza umuhimu wa Chuo kuepuka kuwa taasisi ya kitaaluma pekee na badala yake kujikita katika shughuli nyingine muhimu kama vile utafiti na ushauri wa kitaaluma. Mhadhiri, Dkt. Eng. David Kimera kutoka Uganda, aliishukuru menejimenti ya Chuo cha Bandari kwa ukaribisho mzuri na kueleza kuwa ana imani kwamba ziara hiyo ya siku nne (4) itakidhi matarajio yao.

bandari collage 18

bandari collage 11

 

Bandari college 1