Chuo cha Bandari kimefunga rasmi mafunzo ya Waendesha mtambo wa Reach-Stacker. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 11 Oktoba 2024.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Bw.Franco Mwakatage ameishukuru Menejimenti ya GGML kwa kuendelea kukiamini Chuo kwa kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Mgodi huo na kuwapongeza washiriki walio hitimu kwa kuzingatia yale waliyofundishwa ili kuongeza ufanisi na kuleta tija kiwandani kama ilivyo matarajio ya menejimenti.
Naye mwakilishi wa Meneja mafunzo wa GGML Bw.Sebastian Malunde amekipongeza Chuo kwa kuboresha utoaji wa huduma zake siku hadi siku.
Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Kitengo cha Supply Chain wa GGML Bw.Rwechungura alikishukuru Chuo kwa mafunzo mahiri ya uendeshaji salama wa mitambo yaliyotolewa na Wakufunzi wenye weledi katika ufundishaji wa mitambo hiyo.