Bandari College
+255-22-2857114   pbc@ports.go.tz

Katika kutekeleza jukumu la kimsingi la utoaji mafunzo ya kujenga uwezo kwa wakufunzi wa vyuo, Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) inaendesha mafunzo ya siku mbili (2) ya "Train of Trainers"  kwa wakufunzi wa Chuo cha Bandari kuanzia tarehe 21 Agosti 2024.

IMG 20240821 WA0040 

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na EACOP kwa ajili ya maprofesa, wahadhiri na wakufunzi kutoka vyuo vikuu na vile vya kati vya Tanzania ikiwemo Chuo cha Bandari, mafunzo hayo yamelenga kuwajengea na kuwaongozea uwezo washiriki katika masuala yanayohusu teknolojia mpya katika eneo la uhandisi.

IMG 20240821 WA0113

 

Wakufunzi hao wanapata mafunzo ya Control Valves kutoka kwa mwezeshaji Ndg. Balamurali Krishnakumar wa kampuni ya Emerson Contractors.

Chuo cha Bandari ni chuo cha kimkakati ambacho kinaandaa wataalamu wenye uwezo wa kushiriki katika miradi mikubwa ya Kitaifa inayoendelea.

Chuo pia kimekua kitovu cha kuwaandaa wataalamu wanaosimamia miradi katika sekta ya ujenzi na uchukuzi. Hivyo mafunzo haya yanayotolewa na EACOP ni mkakati wa kuongeza ubobezi katika eneo la utoaji mafunzo kwa wanafunzi wanaojiunga na Chuo cha Bandari.

IMG 20240821 WA0115