Chuo cha Bandari kinaendelea kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa taasisi mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi.
Kwa kupitia madarasa yaliyopo katika Bandari ya Tanga, washiriki wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD) wamepatiwa mafunzo ya forklift operator.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Bandari Tanga kuanzia tarehe 05 Agosti 2024 hadi 09 Agosti 2024.